Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 8:04:47
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episódios
-
Nchi za Afrika mashariki zawasilisha bajeti, serikali mpya DRC yazinduliwa
15/06/2024 Duração: 20minTunayoangazia ni pamoja na kutangazwa kwa badgeti ya mwaka 2024/2024 kwenye nchi za jumuia ya Afrika mashariki, serikali ya mwanamke wa kwanza aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu mpya huko DRC ilizinduliwa wiki hii, mauaji ya ADF huko Lubero mashariki mwa nchi hiyo, kifo cha makamu rais wa Malawi katika ajali ya ndege, lakini tutaangazia yaliyojiri Afrika Magharibi, kabla ya kuelekea kwengineko duniani
-
Mapigano Kanyabayonga DRC, katibu mkuu mpya wa EAC, na mengineyo
08/06/2024 Duração: 20minMakala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa afrika huko Korea Kusini, hali ya wasiwasi kutanda kwenye mji wa Kanyabayonga, na mashirika kadhaa ya misaada kuanza kuhama, Burundi na kampeni ya kuvunja ndoa zisizorasmi, hotuba ya rais wa Uganda Yoweri M7, siasa za nchini Kenya, juhudi za kimataifa kuhusu amani ya Sudan, hali ya kisiasa Afrika kusini baada ya uchaguzi, hali ya usalama huko Gaza na siasa za Marekani
-
Serikali yatangazwa DRC, ndege aliyokodisha rais Ruto yazua gumzo na mengineyo
01/06/2024 Duração: 20minTunayoangazia wiki hii ni pamoja na uteuzi wa baraza jipya la mawaziri huko DRC pia kuendelea mapigano eneo la mashariki mwa nchi hiyo, mchakato wa uchaguzi wa mwezi Julai nchini Rwanda, safari ya rais wa Kenya William Ruto huko Marekani na ndege aliyotumia ilivyozua gumzo, juhudi za kimataifa kuhusu amani ya Sudan, uchaguzi wa Afrika kusini, Hali ya Gaza na siasa za Marekani.
-
Marekani yataka Kenya kujiunga na NATO, mapigano mashariki yaendelea DRC
25/05/2024 Duração: 20minMakala imeangazia ziara ya rais wa Kenya William Ruto nchini Marekani, Uingereza na mpango wa kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda, Jeshi la Congo FARDC laimarisha mapambano kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo, uchaguzi kule Afrika kusini, siasa za Chad baada ya kuapishwa kwa Mahamat Idriss Debi, siasa za Afrika Magharibi, hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israeli B-Netanyahu, na viongozi wa Hamas pia mengineyo