Changu Chako, Chako Changu
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 7:40:25
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Episódios
-
Changu Chako Chako Changu tasnia ya ulimbwende sehemu ya kwanza Agost 04 2024
04/08/2024 Duração: 20minKaribu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea mambo mbalimbali ya utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sanaa ya Ulimbwende au Model, na kwenye la parler francophone nitakuletea shughuli zinazoendelea kwenye vituo vya Alliance francaise za ukanda kipindi hiki cha michuano ya Olympiki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue.
-
Historia ya kabila la Wabukusu pamoja na sanaa ya muziki kutokea kwa Bendi ya An Noor
21/07/2024 Duração: 20minKaribu kwenye makala ya changu chako ,chako changu juma hili ukiwa nami Florence Kiwuwa. Na kwenye kipengele cha historia hii leo tutaangazia historia ya kabila la Waluhya wanaofahamika kama wabukusu kisha kwenye kipengele chetu cha pili cha LeParle Francophone tutaangazia maonyesho ya Taarab yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance France kisha tutamalizia na mwanamuziki wa Kenya almarufu kama Freshely Mwamburi.
-
Matumizi ya lugha ya kiswahili katika enzi ya Kijiditali
16/07/2024 Duração: 20minKiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 afrika mashariki na kwenye makala haya ya changu chako,chako changu ,Florence Kiwuwa amefanya majadiliano na wanafunzi katika chuo kikuu cha Multmedia ili kujua kuhusu mchango wa lugha hii katika kuendeleza utamaduni na utengamano na vilevile katika kipengele cha muziki amemuangazia mwanamuziki wa Tanzania Harmonize.