Afrika Ya Mashariki

Changamoto za raia wa Afrika Mashariki kupata maji kwa ukaribu

Informações:

Sinopse

Makala ya Afrika mashariki ikiangazia juu ya namna wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki wakiwa katika mkwamo wakupata katika huduma ya maji kwa ukaribu licha uwepo wa vyanzo vikumbwa vya maji. Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Afrika mashariki, Maziwa makubwa yote mawili kwa maana ya ziwa Victoria na Tanganyika, na hatimaye, Mto White Nile hutegemea vyanzo vya maji vya kikanda vinavyojulikana kama  Minara ya maji Water Towers ya eneo hilo.Minara ya Maji ya Afrika mashariki ni mkusanyiko wa mazingira ya milimani na mabonde ya mito yanayohusiana.Maeneo haya yana ushawishi mkubwa kwa hidrolojia ya kikanda na mizunguko ya hali ya hewa duniani.Licha ya uwepo wa minara hii bado serikali za wanachama wa jumuiya hii zipo katika mkwamo wakufikisha huduma za maji kwa wananchi walio wengi.