Habari Za Un
03 OKTOBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:11:16
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kumulika ugonjwa wa homa ya nyani au mpox. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za machafuko Lebanon, Haiti na Sudan. Katika kujifunza Kiswahili Onni Sigalla anafafanua maana ya neno “NGEJA” Mashariki ya Kati, nchini Lebanon hali inaendelea kuwa tete amesema mratibu maalum wa Umoja wa mataifa nchini humo Jeanine Hennis Plasschaert. Kupiti ukurasa wake wa mtandao wa X amesema umekuwa usiku mwingine wa kutoka kulala mjini Beiruti milipuko ikighubika mji huo bila tahadhari, raia wakikumbwa na taharuki bila kujua mustakbali wao.Mtaalamu mhuru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Sudan Radhouane Nouicer, leo ametoa wito kwa jeshi la Sudan (SAF), Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na wanamgambo wenye silaha kuchukua hatua za haraka kuhakikisha ulinzi wa raia mjini Khartoum, huku kukiwa na ongezeko la uhasama na ripoti za kutatanisha za mauaji ya kiholela.Na zaidi ya watu laki 7, sasa ni wakimbizi w