Habari Za Un

Vivian Joseph: Taasisi ya Watoto Afrika ni fursa kwa kila mtoto kufikia uwezo wake

Informações:

Sinopse

Moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa  ya maendeleo endelevu SDGs ani lengo namba 4 la kuhakikisha elimu bora kwa kila mtoto. Hata hivyo bado katika nchi  nyingi hususan zinazoendelea watoto wengi hasa wenye ulemavu wanakosa fursa za kufikia uwezo wao kutokana na changamoto za kupata elimu iwe rasmi au isiyo rasmi na hivyo kusalia nyuma. Umoja wa Mataifa umekuwa ukizichagiza nchi na jamii kuchukua hatua  ili kubadili mwelekeo huo. Nchini Tanzania kijana Vivian Joseph ni miongoni mwa walioitikia wito wa hatua na akaanzisha taasisi isiyo ya kiserikali ya Watoto Afrika Initiative nili kusaidia watoto  wenye changamoto ikiwemo ulemavu waweze kupata fursa hiyo ya elimu. Katika makala hii amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa kuhusu taasisi hiyo akianza kwa kufafanua wanachokifanya.