Habari Za Un
02 OCTOBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:09:59
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mokuu katika Siku ya Kimataifa ya Kutokuwa na Ghasia, na waandishi wa habari katika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu. Makala inatupeleka Tanzania kuangazia taasisi ya watoto Afrika Initiative, na mashinani inatupeleka Amhara, Ethiopia, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokuwa na Ghasia, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa amezitaka nchi kubadilisha kuwa uhalisia ahadi za kuleta amani duniani walizojiwekea katika Mkutano wa Zama zijazo uliokamilika hivi majuzi hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Umoja wa Mataifa kila uchao unapigia chepuo wadau mbali mbali wakiwemo waandishi wa habari kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs ili sio tu yaweze kufahamika bali pia wale wanaowajibika kuyatekeleza wafanye hivyo ili hatimaye maisha ya wananchi yawe bora na si bora maisha.Makala inatupeleka Tanzania kuangazia taasisi ya watoto Afrika Initiative, iliyoanzishwa ili kuwasaidia watoto hususani vijana balehe. Je,