Habari Za Un

Ugonjwa wa Mpox ‘umepoteza’ watoto wanne wa familia moja DRC

Informações:

Sinopse

Ukisikia makovu yasiyofutika ni ya simulizi hii utakayoisikia kuhusu familia moja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupoteza watoto wanne kutokana na ugonjwa wa homa ya nyani au mpox huku mustakabali wao ukisalia mashakani kwani bado hawafahamu hali itakuwa vipi kwenye familia yao, baba na mama wakipambana na ugonjwa huo. Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyochapishwa kwenye mtandao wa Instagram unatupeleka Mbandaka, mji ulioko jimboni Equateur, kaskazini-magharibi mwa DRC.Dkt. Douglas Noble Mkurugenzi Mshiriki, UNICEF ndiye mwenyeji wetu hapa kwani ametembelea kituo cha matibabu ya mpox hapa Mbandaka.“Tuko hapa Mbandaka, ambapo kuna idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa mpox. Tumetembelea kituo cha matibabu, na ni huzuni kusikia hadithi ya familia moja yenye watoto sita, ambapo wanne walifariki dunia kwa  mpox. Watoto wawili wako vizuri kwenye kituo cha watoto. Baba na mama bado wako kituo cha matibabu”"Ni kwa kuzingatia madhara ya ugonjwa wa mpox kwa wat