Habari Za Un

Wiki mbili za kusaka usalama DRC, mkimbizi asimulia madhila na atakacho.

Informações:

Sinopse

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesalia katika mgogoro kwa miaka mingi, hali ambayo imewasababishia raia mateso ya hali ya juu zaidi yakiwemo mauaji, utekaji nyara, na kuteketezwa kwa nyumbaa zao. Mapigano hayo pia yamewafungisha viragozaidi ya watu milioni 6.4 nchini humo, na kulazimisha familia kutafuta usalama katika makazi ya muda yaliyojaa pomoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu na ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwiba kwa wakimbizi hawa wa ndani.  Cicey Kariuki na taarifa zaidiRusayo ni eneo lililo na makazi ya muda ya wakimbizi   mjini Goma katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Miongoni mwa  wakimibizi wa ndani wanaishi kwenye makazi haya ni Sebororo, mwanamke mwenye  miaka 38 akitembea na watoto wake.Sebororo pamoja na wananawe watano wanaishi kwenye makazi ya pamoja na familia nyingine 90 huku wakisubiri kutengewa nyumba katika eneo hilo. Mama huyu anaeleza jin