Habari Za Un
UN: Lebanon inakabiliwa na zahma kubwa wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:02:01
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO linasema hali nchini Lebanon ni janga la kibinadamu watu wengi wamejeruhiwa , wengine kupoteza maisha na mfumo wa afya umelemewa.Kupitia ukurasa wake wa X Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema katika jitihada za kuwasaidia waathirika ndege ya kwanza ya msaada wa vifaa vya kitabibu vya upasuaji, dawa na vifaa tiba vingine imewasili mapema leo mjini Beiruti na vifaa hivyo vitatosha kuwatibu maelfu kwa maelfu ya watu na kuokoa maisha yao na ndege nyingine mbili zitawasili baadaye leo.Kwa upande wake Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema maelfu ya watu wanaendelea kukimbia mashambulizi ya makombora ya Israel na wengine wakivuka