Habari Za Un

Awamu ya 2 ya chanjo dhidi ya Polio Gaza yaanza licha mashambulizi

Informações:

Sinopse

Mashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio  Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe. Naanzia eneo la kati mwa ukanda wa Gaza ambako asubuhi ya leo Jumatatu awamu ya pili ya chanjo dhidi ya polio imeanza ikilenga watoto 591 700 wenye umri wa chini ya miaka 10,  watakaopatiwa dozi ya pili ya chanjo hiyo kufuatia kuthibitishwa kwa polio Gaza mwezi Agosti mwaka huu.Chanjo inatolewa licha ya ripoti za makombora kurushwa kwenye shule moja iliyogeuzwa makazi ya wakimbizi huko Nuseirat na katika hospitali moja huko Deir Al-Balah ambako mahema kadhaa yaliteketezwa kwa moto wakati watu wamelala.Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, Louise Wateridge akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema,&n