Habari Za Un

24 OKTOBA 2024

Informações:

Sinopse

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada inayotupeleka nchini Kenya kuzunguza na uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mada tofauti ikiwemo uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno HEKEMUA.Uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) uliotolewa leo jijini New York, Marekani katika Siku ya Kimataifa ya Polio, unaonesha kwamba asilimia 85 ya watoto 541 waliokumbwa na polio duniani mwaka wa 2023 wanaishi katika nchi 31 zenye mifumo dhaifu, zinazokabiliwa na mizozo, halikadhalika zilizo hatarini.Umoja wa Mataifa ulijengwa na ulimwengu, kwa ajili ya ulimwengu, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku ya leo ya Umoja wa Mataifa.Na leo Oktoba 24 huko Kazan nchini Urusi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa viongozi wa kundi la BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini akisisit