Habari Za Un

Mbinu bora za malezi zimebadilisha maisha katika Wilaya ya Kyegegwa - UNICEF Uganda

Informações:

Sinopse

Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto  UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana. Leo tuko katika wilaya ya Kyegegwa nchini Uganda ambapo, kwa msaada wa UNICEF,  wafanyakazi wa kijamii, kamati za ulinzi na ustawi  wa watoto, na kikosi cha polisi; wote wamepewa mafunzo mwafaka ili kuhakikisha ulinzi wa watoto unaofaa na wa kudumu, na tunakutana na Agnes Karungi mama mwenye umri wa miaka ishirini na  mmoja wa wanufaika wa mradi wa malezi bora. Mbali na kukumbana na changamoto za kuwa mama kijana, mwanaye Agnes, ni mwenye ulemavu na zaidi ya hayo a