Habari Za Un
Nadipo: Asante WFP kwa mradi wa mizinga ya nyuki sasa familia yangu inatabasamu
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:03:20
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”