Habari Za Un
Esneda kutoka jamii ya Yukpa asema haogopi vitisho kutetea eneo la jamii yao ya asili nchini Colombia
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:03:39
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia imevumilia miongo kadhaa ya migogoro na watu kutawanywa inayosababishwa sio tu na mabadiliko ya tabianchi mila kandamizi bali pia kupotea kwa viumbe hai na hivyo kutishia maisha yao. Esneda Saveedra, Kiongozi wa jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia akiwa anazungumza akiketi ndani ya msitu na kando ya mto Maracas., anasema hana hofu ya kutetea ardhi hii.Ardhi anayozungumzia ni eneo hilo la mto Maracas anayotetea dhidi ya vitisho kutoka kwa waharibifu wa mazingira kufuatia yale yaliyojadiliwa katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa bayonuai, COP16 uliomalizika Ijumaa iliyopita huko mjini Cali nchini Colombia."Sina hofu ya kutetea ardhi hii. Yale niliyopitia kama mtoto, changamoto zote hizo, yalinipa nguvu, yalinipa ujasiri, na yakaondoa hofu yangu."Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inatupatia taswira ya juu ya eneo la makazi ya jamii ya Yukpa, msitu mnene na kisha kwenye mto Maracas, shughuli zinaende