Habari Za Un
23 DESEMBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:10:00
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher mashariki wa kati, na uwezeshaji wa vijana katika sekta ya kilimo nchini humo. Makala inatupeleka nchini Zimbabwe na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher akihitimisha ziara yake ya kwanza katika eneo la Mashariki ya kati tangu hivi karibuni alipochukua wadhifa huo ameeleza kuwa alichokishuhudia katika ukanda huo ni hali tete.Mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Zimbabwe kumulika nuru iliyofikia wakulima baada ya Umoja wa Mataifa kuona jinsi mabadiliko ya tabianc