Habari Za Un

18 DESEMBA 2024

Informações:

Sinopse

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya wahamiaji duniani ikimulika mchango wa wakimbizi na wahamiaji katika ukuaji wa kiuchumi na kukuza jamii zao n aza wenyeji. Tutasikia kutoka mkuu wa IOM, Katibu Mkuu wa UN na wahamiaji Burundi na Chad. Pia tunaangazia ufugaji nyuki Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo.Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM.Makala i