Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 3:59:42
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Episódios
-
Dampo la Nkumba- Tishio kwa ziwa Victoria na maisha ya jamii za Uganda
26/12/2024 Duração: 10minMakala haya yanazungumzia jinsi dampo la Taka la Nkumba nchini Uganda limekuwa tishio la kimazingira kwa ziwa victoria ambalo ndilo chanzo kuu cha mto Nile.Baada ya dampo la Kiteezi jijini Uganda kuporomoka Agosti 9 mwaka wa 2024 na kuwauwa watu kadhaa,serikali nchini humo ilitoa amri taka zote kutoka Kampala ielekezwe Nkumba karibu na ziwa ,hatua hiyo ikiongeza uchafuzi zaidi wa mazingira .
-
Mwanzo mpya: vijana wa Pwani ya Kenya wajijenga upya kupitia kazi za mazingira
17/12/2024 Duração: 10minKatika miji ya pwani ya Kenya, vita dhidi ya uraibu vimepata mwelekeo mpya wa kusisimua. Kupitia miradi ya kimazingira, vijana kutoka vituo vya kuwarekebisha tabia hawajizuia tu na mihadarati, bali wanabadili jamii zao pia kupitia miradi hiyo. Mwanahabari wetu Victor Moturi alitembelea Mtopanga, Kaunti ya Mombasa, ambako vijana wamepata matumaini kutokana na utunzaji wa mazingira huku wakipata riziki.
-
Wataalam wa mazingira: Kuchakata plastiki sio suluhu ikiwa nchi zinazalisha zaidi
10/12/2024 Duração: 10minMkutano wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki ulikamilika mwanzoni mwa Disemba 2024 bila mwafaka kufikiwa, wataalam wa mazingira wakisema pendekezo la kuchakata plastiki wakati nchi nyingine zikiendelea kuzalisha sio suluhu la tatizo hilo. Kwenye makala hii leo tunaangazia athari za plastiki kwa afya na mazingira, suluhu zinazopendekezwa lakini pia kupata ufafanuzi zaidi kilichokwamisha kupatikana kwa mkataba wa kumaliza tatizo linalosababishwa na uchafuzi wa plastiki.
-
COP29: Wanamazingira wapendekeza ufadhili zaidi kwa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
19/11/2024 Duração: 09minMkutano wa hali ya hewa COP29 ukiendelea nchini Azerbaijan, masuala yanayoibua changamoto ni ufadhili, mchakato wa kuondokana na mafuta kisukuku, athari ambazo zimekumba bara la Afrika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kuongezeka kwa viwango vya joto lakini pia suluhu zinazopendekezwa na wataalam wa mazingira. Kauli mbiu ya mwaka huu kwenye mkutano wa COP29 ni uwajibikaji wa ufadhili haswa kutoka mataifa tajiri ambao wanachangia kwa viwango vikubwa uchafuzi wa mazingira wakati athari zake zinaathiri nchi zisizojiweza na shirika la mazingira la Greenpeace Africa linapendekeza mustakabali wa nishati mbadala na haki ya hali ya hewa kwa Afrika.Kwa mengi zaidi bonyeza ili kusikiliza makala.
-
Ripoti ya mazingira ya UNEP kuhusu pengo la uzalishaji wa gesi chafu duniani 2024
31/10/2024 Duração: 10min -
Jamii Pwani ya Kenya wapinga mradi wa nyuklia kutokana na athari kwa mazingira
29/10/2024 Duração: 09min -
DRC:Jamii ya mbilikimo wakemea uharibifu wa misitu unaofanywa na makundi ya waasi
09/10/2024 Duração: 10min -
-
Siku ya kimataifa ya kufanya usafi wa mazingira na matumlizi ya teknolojia
23/09/2024 Duração: 10minKatika dunia ya sasa ambapo ukuaji wa teknolojia ni wa kasi ya juu, wabunifu katika jamii za pwani nchini Kenya, wamekumbatia matumizi ya teknolojia katika kupiga jeki juhudi za kupunguza taka kwenye mazingira wanayoishi.
-
Wahifadhi wahofia kudidimia kwa tembo aina ya "Super Tusker'
06/09/2024 Duração: 09minWanasayansi na wahifadhi wameibua hofu ya kutokomea kabisa kwa tembo aina ya "Super Tusker" ambaye pembe yake moja ina kilo takriban 45, ikiwa hatua hazitachukuliwa ili kuzuia uwindaji wao.Katika mbuga ya Amboseli inayopakana na Kenya na Tanzania, ndovu hawa wamebaki kumi pekee.
-
Mchango wa mashirika yasio ya kiserikali kuwezesha upatikanaji wa maji safi kwa jamii nchini Kenya
06/09/2024 Duração: 10minKatika maadhimisho ya wiki ya maji duniani 2024, makala haya yameangazia mradi wa WASH unaofanywa na shirika la SHOFCO mtaani Kibera, kusambaza maji safi ya matumizi kwa wakaazi wa kitongoji hicho chenye changamoto za upatikanaji wa maji safi.
-
Matumizi ya taka za chupa za plastiki kuendeleza kilimo bila mchanga(Hydroponic farming)
12/08/2024 Duração: 09minKundi la vijana la Vision Bearers la mtaani Mathare, jijini Nairobi linavyotumia taka za chupa za plastiki kuendeleza kilimo bila mchanga(Hydroponic farming)
-
Kenya: Namna mabaki ya ngozi ya samaki yanavyotumiwa kuhifadhi mazingira
05/08/2024 Duração: 09minKwa miaka mingi taka inayotoka kwa samaki na viumbe vingine kwenye ziwa, imekuwa ikichafua mazingira na kusababisha samaki wengi kukosa hewa ya oxigeni hivyo kufariki na kusababisha hasara kubwa.Hata hivyo wenyeji sasa wengi wao vijana wameanza kutumia taka hizo kutengeza bayogesi na bidhaa zingine kama vile viatu,nguo,begi mifuko na kadhalika hivyo kubuni ajira na kuinua uchumi. Katika fuo za Dunga kando na ziwa Victoria kaunti ya kisumu nchini Kenya,wafanyabiashara hapa wanatumia bayogesi kukaanga samaki na kuwauzia wateja wanaotalii êneo hili.Bayogesi hii inayotengenezwa kutokana na mabaki ya samaki ,imewafaidi wenyeji wa hapa kupunguza gharama ya matumizi vile vile kutunza mazingira. Caroline Achieng ni mfanyabiashara wa samaki.“Tunadumisha usafi kwa sababu wageni wanakuja hapa lazima tudumishe usafi ndio mazingira yetu yasiharibike,mradi huo umesaidia sana kwa sababu wametusaidia kuchukuwa hizi takataka za samaki kama matumbo,wanatengeneza nayo bayogasi hivyo kupunguza uchafu”alisema Caroline Achieng m
-
Uhifadhi wa mbegu za kitamaduni na sera zinazotishia mapato ya wakulima wadogo nchini Kenya
29/07/2024 Duração: 10min -
Uhifadhi wa mbegu za kitamaduni na kiasili na shirka la Seed Savers Network
22/07/2024 Duração: 10min -
Ugeuzaji wa taka za plastiki kuwa matofali maalum(Cabro) inayotumika kutengeneza barabara
17/06/2024 Duração: 10minJuma hili katika makala ya mazingira leo dunia yako kesho, mwandishi wetu wa Goma Benjamin kasemabe, ametuandalia ripoti ya namna mjasiriamali Irene maroy anavyogeuza taka za plastiki kuwa matofali maalum maarufu kama Cabro inayotumika kutengeneza barabara.
-
Uboreshaji wa ardhi, kuimarisha ustahimilivu kwa ukame, na kupambana na kuenea kwa majangwa
12/06/2024 Duração: 09min -
Mradi wa Sola katika kisiwa cha Ndeda, nchini Kenya, waleta mabadiliko kwa wakaazi
21/05/2024 Duração: 09min -
Katika makala haya utafahamu kuhusu vimbunga na athari zitokanazo na vimbunga
20/05/2024 Duração: 10min -
Majadiliano kuhusu mkataba wa kisheria wa kimataifa kudhiti uchafuzi wa taka za plastiki
14/05/2024 Duração: 10min