Informações:
Sinopse
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episódios
-
Botswana : Chama tawala chasalimu amri
05/11/2024 Duração: 09minKatika makala haya tunajadili kilichotokea nchini Botswana ambapo Chama tawala Democratic Party, ambacho kimekuwa madarakani tangu enzi za ukombozi kwa maika 58, kimekubali kushindwa na kukabidhi madaraka kwa upinzani, Duma Boko akiapishwa kuhudumu rais kama rais wa sita wa Botswana. Je mataifa mengine ya Afrika yenye vyama vya ukombozi madarani yanaweza jifunza nini kutokana na uchaguzi wa Botswana?Ndilo swali Tumekuuliza na haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Africa: Uturuki yashiriki mkutano na Africa kuimarisha uhusiano
05/11/2024 Duração: 09minTaifa la Uturuki limefanya mkutano na viongozi wa Africa, nchi hiyo ikilenga kuimarisha uhusiano wake na Africa. Lakini je kuna la ziada katika mkutano huu. Haya hapa baadhi ya maoni yenu.
-
-
Kenya: pendekezo la kufanya marekebisho ya katiba kuongeza muda rais na wabunge madarakani
29/10/2024 Duração: 10min -
-
Kuongezeka kwa ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana kwenye maeneo yenye mizozo
02/10/2024 Duração: 09min -
Ripoti yaonesha kushuka kwa uaminifu wa uchaguzi kati ya mwaka 2020 na 2024 katika nchi 21 Afrika
30/09/2024 Duração: 10min -
Kwa nini bado usawa wa kijinsia haujafikiwa katika mataifa mengi ya Afrika
26/09/2024 Duração: 09minRipoti ya hivi karibuni ya umoja wa mataifa ,kuhusu usawa wa kijinsia, takwimu zinaonesha hatua kupigwa lakini changamoto bado zimesalia.
-
Majengo duni yanayoporomoka na kusababisha majanga barani Afrika
25/09/2024 Duração: 09minWiki iliyopita watu kadhaa walipoteza maisha kufuatia jengo liloporomoka nchini Sierra Leone
-
Ajali za boti katika mataifa ya Afrika yakiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
24/09/2024 Duração: 10minWatu wengi wameendelea kupoteza maisha katika majanga ya majini
-
Mwanae rais wa Uganda Jenerali Muhoozi asema nchi hiyo itaongozwa na polisi au jeshi
23/09/2024 Duração: 10minJenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema hatowania urais ila Uganda itaendelea kuongozwa na polisi au jeshi baada ya rais Museveni Juma lililopita mtoto wa Rais wa #Uganda pia mkuu wa majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa nchi hiyo itaongozwa na mwanajeshi au polisi baada ya baba yake kuondoka madarakani.
-
Tanzania: Rais Samia awaonya mabalozi
19/09/2024 Duração: 09minkatika makala haya tunajadailki hatua ya rais wa rais wa #Tanzania #SamiaSuluhuHassan , kuwaonya makutoa ya pamoja taarifa kulaani matukio ya utekaji na mauaji dhidi ya wakosoaji wa Serikali yake. Je unafikiri kauli Samia ni sahihi?Ndilo swali tumekuuliza, na haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Africa : Ukosefu wa ajira wachangia uhalifu miongoni mwa vijana
18/09/2024 Duração: 09minKatika makala haya tunajadili kinachoendelea katika mataifa mengi ya Afrika kuendelea kushuhudia ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, hii likichangia kwa kiasi kikubwa uhalifu. Je Wewe unafanya nini ili kupata riziki ya kila siku ?Ndilo swali tumekuulizaHaya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Africa : Ndoa zinaendelea kuvunjika haraka kinyume na awali
17/09/2024 Duração: 09minKatika makala haya tunajadili misururu ya kuvunjika kwa ndoa za siku hizi hili haliathiri tu watu wa kawaida bali pia watu maarufu katika jamii zetu. Je unafikiri nini kinachangia ndoa za siku hizi kuendelea kuvunjika haraka kinyume na zamani?Ndilo swali tumekuuliza, na haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Sudan Kusini : Serikali yaarisha uchaguzi kutokana na shinikizo za wadau
16/09/2024 Duração: 09minkatika makala haya tunajadili hatua ya serikali ya Sudan Kusini juma lililopita kutangaza kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike mwezi Desemba mwaka huu. Uchaguzi huu sasa ukisongezwa mbele kwa miaka miwili baada ya shinikizo la ndani na nje.Je huu ni uamuzi sahihi kwa Sudan Kusini?Haya hapa baadhi ya maoni yako
-
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia chochote kile
01/09/2024 Duração: 10minKila ijumaa inapata nafasi kuchangia mada yoyoyte ndani ya makala Habari Rafiki, makala ambayo huenda hewani ndani ya rfi Kiswahili kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Skiza kufahamu maoni ya waskilizaji kuhusiana na mada mbalimbali.
-
Sudan : UN yatathimini kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wa Sudan
29/08/2024 Duração: 09minKatika makala haya tunajadili hatua ya umoja wa mataifa kusema unatathimini kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wawili nchini Sudan ambao wamekuwa kwenye vita kwa zaidi ya miezi 17. Je unafiriki kutangazwa kwa vikwazo dhidi ya majenerali wa Sudan kutasitisha vita nchini Sudan? Unahisi jumuiya ya kimataifa imesaidia, kutatua mizozo Africa, ndio maswali tumekuuliza. Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Kenya : Mataifa ya Africa yakosa kuzingatia katiba
28/08/2024 Duração: 09minKwenye makala ya Habari Rafiki leo tunajadili kilichofanyika nchini Kenya, ambapo taifa hilo la Africa mashariki limeadimisha miaka 14 tangu lijipatie katiba ya mwaka 2010, ila imekuwa vigumu kwa serikali kutekeleza baadhi ya vipengee vya katiba hiyo. Unafiriki nini huzuia serikali yetu kuttotekeleza katiba?Ndilo swali tumekuuliza, na haya maoni yako.
-
Africa : Inasubiri chanjo ya Mpox kutoka ulaya
27/08/2024 Duração: 09minkatika makala ya Rabari Rafiki, leo mskilizaji tunajadili hatua ya Mataifa ya Afrika yalioathirika na ugonjwa Mpox kuendelea kusubiri chanjo kutoka kwa mataifa ya magharibi ili kuwapa raia walioathirika. Je unafikiri kwa nini hadi sasa Afrika haiwezi tegeneza chanjo yake? Ndilo swali tumekuuliza na haya maoni yako.
-
Sudan : Kiongozi wa kijeshi asema yuko tayari kwa vita na hatashiriki mazungumzo ya amani
26/08/2024 Duração: 09minKatika makala haya tunajadili hatua ya kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, kusema hataki mazungumzo yoyote yatayohusisha wapiganaji wa RSF, akisema jeshi liko tayari kupigana hata kwa miaka 100. Matamshi yake yamekuja wakati huu Marekani ikiongoza juhudi za kupata mwafaka wa mani kati yake na vikosi vya RSF.