Informações:
Sinopse
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episódios
-
Nchi zote pamoja na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN yanawajibika kukomesha ukaliwaji wa Palestina
18/10/2024 Duração: 02minTume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo.Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa.Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyin
-
Mbegu za asili zinanisaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi - Mkulima
18/10/2024 Duração: 03minShirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linapigia chepuo uwepo wa mifumo ya uzalishaji chakula inayoendana na kila eneo husika, mathalani kilimo kitumie mbegu za asili za eneo husika kama mbinu ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kupata aina tofauti tofauti za mbegu za asili kwa eneo husika kunainua kipato cha wakazi wa vijijini na kuongeza mnepo majanga yanapotokea. Na hicho ndio anafanya mkulima kutoka Tanzania ambaye wakati wa maonesho ya siku ya chakula duniani huko mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania alieleza kwa nini ameamua kuchukua hatua hiyo. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
-
UN Ripoti: Uwezekano wa kifo cha Dag Hammarskjöld kuwa ni hila unaongezeka kutokana na taarifa mpya
18/10/2024 Duração: 02minRipoti nyingine mpya ya tathimini ya uchunguzi wa hali na mazingira ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1961 Dag Hammarskjöld imetolewa leo ikiwa na vipengele vinne vipya vikiongeza uwezekano kwamba kifo hicho cha ajali ya ndege kilikuwa ni hila. Asante Anold kwanza ikumbukwe kuwa hii sio ripoti ya kwanza na huenda isiwe ya mwisho ya kutathimini hali na mazingira yliyochangia ajali ya ndege iliyokatili maisha ya Dag Hammarskjöld tarehe 17 Septemba 1961 akiwa njia kuelekea Congo ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cngo DRC, kujadili usitishwaji wa uhasama ila ni ripoti ya karibuni zaidiRipoti inasema mwenyekiti wa jopo la tathimini ya uchunguzi jaji mkuu wa zamani wa Tanzania Mohamed Chande Othman amepokea taarifa mpya muhimu kutoka kwa nchi wanachama ambazo zinajumuisha maeneo haya Mosi: uingiliaji unaowezekana wa Nchi Wanachama wa mawasiliano husika.Pili: Uwezo wa wanajeshi wa Katanga, au wengine, wa kufanya shambulio linalowezekana kwenye ndege ya SE-BDY,Tatu: kuwepo
-
18 OKTOBA 2024
18/10/2024 Duração: 10minHii leo jaridani tunaangazia eneo linalokaliwa kwa mbavu la Kipalestina, na ndoto Mchezaji kijana wa soka zilizokatizwa na vita katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Kenya, kulikoni?Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina leo imesema mataifa yote na mashirika ya kimataifa, ikiwa ni amoja na Umoja wa Mataifa, wana wajibu chini ya sheria za kimataifa wa kukomesha uwepo haramu wa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, wakati mashambulizi Gaza yakishika kazi na kuongeza madhila kwa raia.Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.Makala inatupeleka Tanzania hususan mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afri
-
Mohamed hajakata tamaa ya kuwa mwanasoka maarufu - Gaza
18/10/2024 Duração: 01minKatika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo. Jua linazama hapa kwenye ufukwe wa Al Mawasi, kwenye bahari ya Mediteranea, wengine wakiwa wanaogelea, na kwa mbali mahema ya waliosaka hifadhi baada ya kufurushwa kaskazini mwa Gaza, mmoja anaonesha mbwembwe za dana dana ya mpira, anajitambulisha."Naitwa Mohamed Abu Jalda, mchezaji wa Klabu ya Rafah Services katika daraja la kwanza. Nilikuwa na ari kubwa ya kuwa mchezaji mkubwa wa soka kama wengine walioko nje ya Ukanda wa Gaza, lakini kutokana na vita, tamaa yangu na maisha yangu yalicheleweshwa, sasa nina zaidi ya miaka 20, nikijaribu kuwa mchezaji wa soka, lakini siwezi kwa sababu naishi Gaza ambapo kuna mapigano ya mara kwa mara. Kila siku nahisi kama ninakufa; Mungu
-
Tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa kwa kuchanganya herufi ‘R’ na ‘L’
17/10/2024 Duração: 01minKatika kujifunza lugha ya kiswahili, matamshi sahihi ya lugha husaidia kufikisha ujumbe sahihi. Kinyume cha hivyo ujumbe utakuwa sivyo ndivyo na ndio maana hii leo, mbobezi wa lugha ya Kiswahili, Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa na mzungumzaji anayechanganya herufi ‘R’ na ‘L’
-
17 OKTOBA 2024
17/10/2024 Duração: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia juhudi za vijana hasa katika kuboresha mifumo ya elimu katika matumizi ya teknolojia ambapo Gloria Anderson, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la TEDI anatufafanulia zaidi.Leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema umaskini umesalia kuwa baa la dunia ukiathiri mamia ya mamilioni ya watu duniani kote.Huko MAshariki ya Kati, awamu ya pili ya utoaji wa chanjo dhidi ya polio imekamilika eneo la kati mwa Gaza, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema watoto 181,429 wamepatiwa. Wengine 148,064 wamepatiwa matone ya vitamini A. Ingawa hivyo vituo vinane vya afya vitasalia wazi ili kuendelea kutoa chanjo kwa familia zilishindwa kufikisha watoto wao katika siku tatu za chanjoMkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amezuri Rwanda kujionea harakati za taifa hilo k
-
Asante WFP sasa najua kuandika na kusoma jina langu – Mkimbizi DRC
16/10/2024 Duração: 03minMbali na usaidizi mkubwa kwa watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro mashariki mwa DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linatoa msaada kupitia miradi iliyo ndani ya mfumo wa kuzuia na kupunguza hatari za unyanyasaji wa kijinsia unaohusishwa na uhakika wa kupata chakula. Takriban wanawake 40 waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi ya Bulengo jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC wamenufaika na mafunzo ya kusoma na kuandika tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024. Walengwa waliojifunza kusoma na kuandika wanashuhudia kwamba yamebadilisha maisha yao. Mwandishi wetu wa habari mashariki mwa DRC, George Musubao alisafiri kutoka Beni hadi Goma katika kambi ya Bulengo kuzungumza na mmoja wao.
-
Kambi ya huduma za macho ya UNICEF yawezesha watoto kuona vema
16/10/2024 Duração: 02minNchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Mmoja wa wanufaika wa juhudi hii ni Candy, msichan wa mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino.Akiwa mwingi wa matumaini, Eric Odhiambo Okeyo, baba mzazi wa mtotohuyo alimpeleka kwenye kambi hiyo jijini Kisumu ambapo alifanyiwa uchunguzi na matibabu.Baada ya kufanyiwa uchunguzi, Candy alielekezwa kwa daktari wa macho ili abaini aina ya miwani ambayo ingemfaa.“Mtoto alipoanza shule niligundua kwamba mwendo wake katika masomo ulikuwa wa polepole sana na pia alikuwa analamika kwamba haoni anachoandika mwalimu. Hata akienda kucheza niliona kwamba alikuwa akifunga macho mara kadhaa. Ilikuwa inanikosesha amani kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa akiteseka,” amesema Eric.Mpango huu wa kielelezo wa UNICEF na wadau wake unashughulikia c
-
16 OKTOBA 2024
16/10/2024 Duração: 09minHii leo jaridani tunaangazi siku ya chakula duniani ikitupeleka jijini Roma Italia kufuatilia maadhimisho yake. Pia tunakupeleka nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanhaha kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Makala tunakwengda nchini DRC na mashinani Sierra Leone, kulikoni?Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la Watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto ikiwemo Candy mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino. Baba yake alifika kwenye kambi hiyo na anatusimulia kupitia video ya UNICEF Kenya.Makala inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
-
Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya chakula duniani yaangazia haki ya chakula salama chenye lishe na cha bei nafuu
16/10/2024 Duração: 01minWashiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Ni maadhimisho ambayo yamewaleta wadau wa kilimo na chakula kutoka kote duniani lakini yanakuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora, FAO inaeleza katika taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa wavuti.Katika hotuba yake ya ufunguzi Mkurugenzi Mkuu wa FAO, QU Dongyu, amesema mifumo ya kilimo cha chakula inabidi "kusaidia wakulima wadogo, wakulima wa ngazi ya familia na wafanyabiashara wadogo katika mnyororo wa thamani ambao katika nchi nyingi ni wa msingi katika kufanya vyakula vyenye lishe, v
-
15 OKTOBA 2024
15/10/2024 Duração: 10minHii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya chakula duniani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatili juhudi za FAO za kuhakikisha haki ya chakula kwa maisha bora na mustakabali bora kwa wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Licha ya mashambulizi, awamu ya pili ya chanjo kwa watoto dhidi ya polio huko Gaza iliyoanza jana imeendelea leo Jumanne eneo la kati mwa Gaza na hadi sasa watoto wapatao Elfu 93 wenye umri wa chini ya miaka 10 wameshapatiwa dozi ya pili.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo linatoa wito wa msaada wa dharura kuepusha janga la kibinamu eneo la kusini mwa Afrika kutokana na ukame uliochochewa na El- Niño.Na ubia mpya wa kutokomeza watu kukosa utaifa umezinduliwa huko Geneva, Uswisi ukilenga kutokomeza hadhi hiyo inayoathiri mamilioni ya watu duniani. Zaidi ya nchi 100, mashirika ya kiraia, taasisi zinazopigia chepuo kuondokana na hadhi hiyo, wanazuoni na wadau wengine wameanzisha ubia huo ikiwa ni kuendeleza kampe
-
Wagonjwa majeruhi wa vita 16 wahamishwa kutoka hospitali ya Kamal Adwan kuwapeleka katika hospitali ya Al-Shifa
14/10/2024 Duração: 03minOperesheni ya vikosi vya jeshi la Israel inayoendeea Kaskazini mwa Gaza kwa njia ya anga na ardhini kukabiliana na wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas yamelifanya eneo hilo kukatwa na sehemu zingine za Gaza, kwa kiasi kikubwa raia wakikosa huduma za msingi kama chakula, elimu na matibabu. Hospitali karibu zote Gaza Kaskazini hazifanyi kazi na iliyosalia ni Kamal Adwan nayo ikitoa huduma kwa kiasi kidogo sana kutokana na ukosefu wa vifaa, wahudumu wa afya na mafuta. Majeruhi wa vita wamezidi uwezo wa hospitali hiyo ndio maana ikaamua kuomba msaada kutoka shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuhamisha majeruhi hao kwenda hospitali Al-Shifa mjini Gaza. Katika makala hii Flora Nducha anamulika zoezi hilo la kuhamisha majeruhi.
-
UNICEF yatoa mafunzo ya kutengeneza sodo kwa kijana mkimbizi wa dani nchini Sudan
14/10/2024 Duração: 02minSodo au taulo za kike, vile vile pedi, ni muhimu kwa wanawake na wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan. Msaada wa kifedha kutoka Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, vilabu vya usafi vya UNICEF, na Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID, vijana wakimbizi wa ndani wanawezeshwa kupata suluhisho kwa changamoto za usafi wanazokutana nazo, wakati wa vita na ukimbizi. Mmoja wa vijana hawa wakimbizi ni Samer mvulana mwenye umri wa miaka 16, ambaye amefundishwa kutengeneza sodo na sasa, anazisambaza bure kwa wanawake na wasichana wakimbizi wa ndani katika jimbo la Atbara, nchini Sudan.Nikataka kujua jinsi Samer anatengeneza sodo hizo…"Nashona kati ya vipa
-
14 OKTOBA 2024
14/10/2024 Duração: 10minHii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya katika ukanda wa Gaza yakiwa ni pamoja na chanjo dhidi ya polio huku mashambulizi ya Israel yakiendelea, na kuwahamisha wagonjwa majeruhi. Pia tunaangazia mchango wa wakimbizi Sudan kwa jamii, na ndoa za utotoni Zambia.Mashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe.Sodo au taulo za kike, vile vile pedi, ni muhimu kwa wanawake na wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani
-
Awamu ya 2 ya chanjo dhidi ya Polio Gaza yaanza licha mashambulizi
14/10/2024 Duração: 03minMashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe. Naanzia eneo la kati mwa ukanda wa Gaza ambako asubuhi ya leo Jumatatu awamu ya pili ya chanjo dhidi ya polio imeanza ikilenga watoto 591 700 wenye umri wa chini ya miaka 10, watakaopatiwa dozi ya pili ya chanjo hiyo kufuatia kuthibitishwa kwa polio Gaza mwezi Agosti mwaka huu.Chanjo inatolewa licha ya ripoti za makombora kurushwa kwenye shule moja iliyogeuzwa makazi ya wakimbizi huko Nuseirat na katika hospitali moja huko Deir Al-Balah ambako mahema kadhaa yaliteketezwa kwa moto wakati watu wamelala.Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, Louise Wateridge akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema,&n
-
FAO yaleta nuru kwa wafugaji walioathiriwa na vita Gaza
11/10/2024 Duração: 03minMwaka mmoja wa vita katika ukanda wa Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji na ndio makala yetu ya leo ikisimuliwa na Assumpta Massoi.
-
Guterres: Ni wakati muafaka sisi kuwasikiliza wasichana
11/10/2024 Duração: 01minIkiwa le oni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akianza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia tarehe mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.“Wasichana wanachangia zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi, VVU” anasema Guterres na kwamba wana uwezekano mara mbili zaidi wa wavulana kukosa elimu au mafunzo. Na ndoa za utotoni bado zimeenea, huku takriban msichana mmoja kati ya watano duniani akiolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Kotekote duniani, mafanikio yaliyopatikana kwa bidii ya usawa wa kijinsia yanafutwa na vita dhidi ya haki za kimsingi za wanawake na wasichana, na kuhatarisha maisha yao. kuzuia uchaguzi wao, na kuweka kikwazo cha mustakabali wa wasichana.Kwa kutumia kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo
-
11 OKTOBA 2024
11/10/2024 Duração: 09minHii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike na juhudi za Umoja wa Mataifa za kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unaofanyika mtandaoni. Makala tunakupeleka katika ukanda wa Gaza, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Makala tunakupeleka Gaza ambapo mwaka m
-
UNICEF nchini Ethiopia yarejesha matumaini kwa manusura wa ukatili wa kingono
11/10/2024 Duração: 01minNchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15. Sauti hiyo ya Nasteyo Sahane Layle, Meneja wa kushughulikia visa vya ukatili wa kijinsia dhidi ya akina mama, watoto na wanawake hapa Gode, jimboni Somali mashariki mwa Ethiopia akisema kuwa kazi kubwa tunayoifanya ni visa vinavyohusu ukatili wa kingono.Ni katika video ya UNICEF iliyochapishwa kuonesha kiza kinachokumba watoto wa kike hususan leo ambayo ni siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.Hapa Gode, UNICEF imeanzisha kituo hicho cha kutoa huduma zote na sasa kimekuwa ni kama eneo salama kwa manusura wa ukatili wa kingono.Anaonekana mmoja wa wasaka huduma kituoni hapa akifika tayari kupatiwa huduma, su