Wimbi La Siasa

Waasi wa M23 wauteka mji wa Ishasha licha ya sitisho la mapigano

Informações:

Sinopse

Wiki hii askari wanaofikia 100 wa DRC, walikimbilia Uganda baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Ishasha ulioko mpakani na Uganda hali ambayo ilijiri wakati sitisho la mapigano lilikubaliwa kati ya DRC na Rwanda mjini Luanda Angola chini ya Upatanisho wa rais wa Angola Joao Laurenco. Kwa nini mapigano yanaendelea licha ya juhudi za kikanda na za kimataifa? Ruben Lukumbuka anazungumza na Francois Alwende, mchambuzi wa siasa za DRC akiwa Kenya, Jean Claude Bambaze, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia wilayani Rutshuru akiwa Goma huko DRC.