Informações:
Sinopse
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episódios
-
Msumbuji : Upinzani wakataa kutambua ushindi wa Daniel Chapo
05/11/2024 Duração: 10minNchini Musumbuji maandamano yamekuwa yakishuhudiwa baada ya upinzani kukataa kutambua ushindi wa mgombea wa chama tawala Daniel Chapo. Aliyekuwa mgombea wa upinzani Venancio Mondlane, amekuwa akisisitiza kwamba alipokonywa ushindi, katika makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Musumbiji.Wachambuzi wa siasa za kimataifa Lugete Mussa Lugete na Felix Arego wanafafanua hali nchini Msumbiji.
-
Kenya : Bunge la Kenya lamuondoa naibu rais afisini
26/10/2024 Duração: 10minNchini Kenya bunge la kitaifa na seneti limeidhinisha kuondolewa afisini kwa naibu rais Rigathi Gachagua, kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kueneza siasa za kikabila. Makala haya yaliandaliwa mapema.
-
Mgogoro kati ya rais na naibu wake nchini Kenya ambao ni mzozo wa kihistoria
23/10/2024 Duração: 10minHatma ya aliyekuwa naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua sasa utaamuliwa na mahakama baada ya mabunge yote mawili kumwondoa madarakani kwa njia ya hoja maalum Hatua ya kuondolewa Gachagua ni dhihirisho ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya rais William Ruto na naibu wake Gachagua ,matukio ambayo si mageni nchini Kenya.
-
Maadhimisho ya mwaka mmoja wa shambulio la Hamas huko Gaza Oktoba 7 2024
09/10/2024 Duração: 10minMakala wimbi la siasa inaangazia maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kundi la Hamas, litekeleze shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa huko Israeli, tukio ambalo lilianzisha vita ambayo imesababisha vifo kwa maelfu ya raia wa Kipalestina na maandamano duniani kote kupinga vita hiyo, wakati huu mzozo huo ukihofiwa kuenea katika mashariki ya kati. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka na waalikwa wake
-
Visa vya utekaji na mauaji ya wanasiasa wa upinzani Afrika Mashariki
11/09/2024 Duração: 10minMakala ya Wimbi la siasa inaangazia tukio la kutekwa na kuuawa, kwa wanasiasa wa upinzani kwenye nchi za Afrika mashariki,tukio la hivi punde likiwa ni kutekwa kwa mwanasiasa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema Ali Kibao, na baadaye alikutwa ameuawa, na matukio haya yanaripotiwa pia nchini Uganda na DRC. Ungana na Ruben Lukumbuka pamoja na waalikwa wake Jawadu Mohamed ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za Tanzania akiwa Daresalaam Tanzania, pia Frankline M wa CMD nchini Kenya.
-
Mzozo wa Ethiopia na Somalia na mchango wa jumuiay aza kikanda kutuliza hali
06/09/2024 Duração: 09min -
Amani ya Sudan bado kitendawili
28/08/2024 Duração: 10minMakala hii imeangazia hali ya kibinadamu inavyoendelea kuwa mbaya ndhini Sudan licha ya juhudi za kimataifa zinzoendelea.Nini kifanyike ili kufikia amani ya kudumu ya Sudan? kwa nini serikali imekataa kukaa meza moja na wapiganaji wa RSF? kuangazia hili, Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa Tanzania, lakini pia Dismas Mokua mchambuzi wa masuala ya kisiasa akiwa Nairobi nchini Kenya
-
Mchango wa Jumuiya ya nchi za SADC katika kutafuta suluhu ya mzozo wa DRC
22/08/2024 Duração: 10minKaribu katika Makala Wimbi la siasa ambapo tunazungumzia Mkutano wa 44 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika uliofanyika Harare, Zimbabwe ambapo viongozi walijadili changamoto zinazolikabili kanda hilo hususan usalama mashariki mwa DRC. Wachangiaji mada ni Alhaj Mali Ali akiwa Paris Ufaransa na Andulkarim Atiki akiwa Dar es salaam Tanzania. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa jukumu la Unyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.Kumbuka kutufollow @billy_bilali
-
Kauli ya rais Kagame kuhusu haja ya kuimarishwa kwa usalama wa kikanda
14/08/2024 Duração: 10minWakati wa kuapishwa kwake, Rais wa Rwanda Paul Kagame alikiri kuwepo kwa haja ya kuimarishwa zaidi kwa usalama katika nchi za Ukanda haswa katika eneo la mashariki ya DRC. Ruben Lukumbuka amezungumza na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuhusu kauli hii.
-
Waasi wa M23 wauteka mji wa Ishasha licha ya sitisho la mapigano
08/08/2024 Duração: 10minWiki hii askari wanaofikia 100 wa DRC, walikimbilia Uganda baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Ishasha ulioko mpakani na Uganda hali ambayo ilijiri wakati sitisho la mapigano lilikubaliwa kati ya DRC na Rwanda mjini Luanda Angola chini ya Upatanisho wa rais wa Angola Joao Laurenco. Kwa nini mapigano yanaendelea licha ya juhudi za kikanda na za kimataifa? Ruben Lukumbuka anazungumza na Francois Alwende, mchambuzi wa siasa za DRC akiwa Kenya, Jean Claude Bambaze, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia wilayani Rutshuru akiwa Goma huko DRC.
-
DRC : Yatangaza mpango wake wa kupunguza idadi ya wafungwa magerezani
03/08/2024 Duração: 09minSerikali ya DRC imetangaza mpango wa kuwapunguza wafungwa katika magareza yake, ili kuondoa mrudiko katika taifa hilo. Katika makala haya wanaharakati wanajadili haki za wafungwa kutoka nchini DRC na Uganda.
-
Ufaransa : Macron afanikiwa kufungia mrengo wa kulia nje ya siasa za Ufaransa
15/07/2024 Duração: 09minNchini Ufaransa licha ya mrengo wa kushoto kuibuka na ushindi kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge, duru ya pili ilikuwa kitendawili kwao baada ya vyama vya mrengo wa ksuhoto kushirikiana na kuzuia vyama vya mrengo wa kulia kupata ushindi. Benson Wakoli anaangazia mbinu alaizotumia rais Emmanuel Macron kuvizuia vyama vya mrengo wa kulia kuibuka na ushindi.Kumsaidia kuangazia hili anaye mchambuzi wa siasa za kimataifa Mali Ali , ambaye yupo Pari Ufaransa, pamoja na Lugete Mussa Lugete akiwa nchini Tanzania eneo la Mwanza.
-
Kenya: Vijana watoa chanzo na suluhu ya ufisadi nchini mwao.
11/07/2024 Duração: 10minSerikali ya rais William Ruto ipo kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa vijana nchini humo, wanaomtaka kuchukua hatua kali, kupambana na ufisadi. Tunaugana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Multi Media nchini Kenya, wanaozungumzia mtazamo wao kuhusu vita dhidi ya ufisadi katika nchi yao.
-
Uchaguzi wa wabunge nchini Ufaransa na mustakabali wa ulaya
03/07/2024 Duração: 10minMakala ya wimbi la siasa imeangazia uchaguzi wa wabunge nchini Ufaransa baada ya kufanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi huo jumapili iliyopita na sasa duru ya pili imepangwa kufanyika julai 07.Uchaguzi huu unaweka wapi siasa za ufaransa, nini mustakabali wa kisiasa kwenye nchi hii, iwapo chama cha mrengo wa kulia cha National Rally kitaibuka mshindi?? Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi.
-
Nini hatima ya maandamano yanayoendelea nchini Kenya ?
26/06/2024 Duração: 11minSiku ya Jumanne, Kenya ilishuhudia maandamano makubwa kupinga mswada tata wa sheria uliopitishwa na wabunge, kuongzeza kodi.Waandamanaji wenye hasira, walivamia majengo ya Bunge jijini Nairobi na kusababisha uharibifu, huku polisi wakiwapiga risasi na kuwauwa waandamanaji.Nini itakuwa suluhu ya mzozo huu ?Tunachambua suala hili na Majeed Ali, mmoja wa vijana wanaounga mkono waandamanaji na Oponyo Akolo Eugene, kutoka Shirika la Wazalendo Movement Afrika, anayepinga maandamano.
-
Kuapishwa kwa Cyril Ramaphona na mstakabali wa serikali mpya ya Afrika kusini
21/06/2024 Duração: 10minMakala hii inaangazia mchakato wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Afrika kusini, baada ya kuapishwa kwa rais Ramaphosa huku chama tawala ANC kikitangaza kufikia makubaliano na vyama vingine, kama DA. Kudadavua hili mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Jijini Daresalaam nchini Tanzania, pia Félix Nabel Arego, mtaalamu wa siasa wa siasa za Afrika kusini akiwa Nairobi Kenya
-
Rwanda yaanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Julai 15 kumchagua rais na wabunge
12/06/2024 Duração: 10minWananchi wa Rwanda wanajiandaa kupiga kura tarehe 15 mwezi Julai kumchagua rais na wabunge.Wiki iiyopita, Tume ya Uchaguzi ilitangaza orodha ya awali ya wagombea urais ambao ni rais Paul Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1994, Frank Habineza kutoka chama cha Democratic Green na Philippe Mpayimana mgombea binafsi.Mwanasiasa na mpinzani wa Kagame, Diane Rwigara, kutoka chama cha People Salvation Movement, ombi lake lilikataliwa. Tunachambua maandalizi ya uchaguzi nchini Rwanda. Wachambuzi wetu ni Edwin Kegoli akiwa Nairobi na Mali Ali akiwa jijini Paris
-
Chama tawala nchini Kenya, kwenye njia panda migawanyiko ikishuhudiwa
31/05/2024 Duração: 09minNchini Kenya, malumbano ya kisiasa yameanza kushuhudiwa kati ya rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua, malumbano hayo yametokana na tofauti za kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027. Kuna hofu kwamba wandani wa rais William Ruto wanawatumia wabunge vijana kutoka ngome ya naibu rais kumtatiza kisiasa hili likiibua malumbano makli ya kisiasa nchini Kenya.Benson Wakoli hapa anachambua swala hili na mchambuzi wa siasa Felix Arego.
-
Jaribio la mapinduzi nchini DRC lazua maswali mengi
22/05/2024 Duração: 10minWimbi la siasa inaangazia kilichotokea Mei 19 jijini Kinshasa ambako vikosi vya jeshi la serikali (FARDC) viilidai kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo.Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jumapili ya Mei 19, lakini sasa tukio hilo limeibua maswali mengi bila majibu. Kudadavua hili, utawasikia Georges Msamali, mtaalamu wa masuala ya kiusalama akiwa Nairobi nchini Kenya, Francois Alwende ni raia wa DRC na mtaalamu wa siasa za DRC.
-
Wimbi la siasa: Madai ya Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu nchini Burundi
17/05/2024 Duração: 10minKwenye Makala haya Ali Bilali akiwa pamoja na wachambuzi wa siasa Mali Ali kutoka Paris Ufaransa na Abdulkarim Atiki wanaangazi kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu hususan uvurumishaji guruneti katika mji wa Bujumbura, tukio la hivi karibuni liligharimu maisha ya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.